KATIBA YA SACCOS
WACHAGA WOTE SACCOS
(WAWOSA) LTD
About Wachanga
wote saving and credits cooperative society (WAWOSA).
Kilianzishwa rasmi tarehe 01/09/2015 kwa juhudi za mwasisi wake
ambaye ni ndugu August August Kessy (Sundaypesa), chini ya uongozi thabiti wa
Maafisa ushirika akiwemo ndugu Emanuel Kessy na ushauri mzuri wa walezi wa
chama Josephina Kessy, Deogratius Lyimo, Rose Mallya pamoja na John Chacky.
Chama hiki cha SACCOS kilianzishwa kwa madhumuni ya kusaidiana
katika shida na raha kama vile:- Msiba, Harusi na Send - off party.
Unaweza kujiunga popote
pale ulipo ndani ya Tanzania au hata nje ya Tanzania kwa kuwasiliana nasi kwa
namba zetu na e-mail yetu ili kuwa mwanachama wetu.
KATIBA YA SACCOS
(a). Ili
kuwa mwanachama wa SACCOS lazima uwe na umri wa miaka (18) na
kuendelea mwenye akili timamu na lazima uwe wa
kabila la Wachaga wa Mkoa wa Kilimanjaro.
(b).
Gharama iliyo pendekezwa kwa kumchangia mwanachama mwenye mahitaji
husika hapo juu ni bei ya gazeti au
vocha yani uwe msiba, harusi au send - off party ni Sh elfu moja 1,000/= tu bila
kujali tukio husika. Hivyo basi gharama hiyo itamsaidia mwanachama kumudu
kuchangia awe mwenye kipato cha juu, kipato cha kati na mwenye kipato cha
chini.
(c ).
Mwanachama atakaye funga ndoa kwa upande wa mwanaume tunamchangia
kiasi
cha sh elfu moja 1000/=.
(e).
Mwanachama atakaye olewa kwa upande wa mwanamke tunamchangia kiasi
cha
elfu moja 1,000/=
(f).
Gharama ya kujiunga kwa mwanachama ni sh. elfu tano tu 5,000/=
(g). Gharama
ya ada ya mwanachama kwa mwezi ni sh. elfu moja tu 1,000/=
unaweza kulipia ada
ya miezi sita yani sh. elfu sita 6,000/= au kulipa pia ada ya mwaka yani
sh. elfu kumi na mbili tu 12,000/= .
(h).
Mwanachama aliyepatwa na ataizo husika anatakiwa kuwasiliana na
mwenyekiti wa SACCOS na mwenyekiti
atawataarifu wanachama wote wa WAWOSA kwenye simu zao
(i). Pindi mwanachama
anapopata taarifa hasa ya msiba kwenye simu yake.
anatakiwa awasilishe mchango wake ndani ya saa ishirini na nne
(24). Hiyo itasaidia maandalizi muhimu ukizingatia msiba hauchukui muda mrefu sana
(j).
Taarifa kuhusu harusi na send - off party mwanachama anapopata
taarifa
anatakiwa awasilishe
mchango wake ndani ya wiki moja.
(k). Mwanachama asiyechangia wenzake ndani
ya matukio matatu yaliyotokea
bila sababu maalumu
atakuwa amejitoa mwenyewe ndani ya chama.
(l).
Mwanachama atachangia tatizo husika tu pindi linapotokea iwe
msiba, harusi
au send-off party.
(m).
Kama hakuna tatizo ndani ya mwezi mzima mwanachama hatohusika na
mchango wowote ule zaidi ya ada yake
ya mwezi.
(n).
Michango yote pamoja na ada ya mwanachama itumwe kupitia namba ya
M-PESA 0756 150093 na TIGO - PESA 0654
238488 jina litakalotokea kwenye simu yako hakikisha ni AUGUST A.
KESSY Mwenyekiti wa chama.
(o)
Kauli mbiu yetu ya chama "CHANGIA NA WEWE UCHANGIWE" au
"UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI
UDHAIFU."
(p).
Kwa maoni, maswali au ushauri tuandikie hapo chini kwenye sehemu ya
maoni au tupigie kwenye namba zetu hapo
juu.
Ahsanteni sana.
No comments:
Post a Comment